Friday 26 January 2018

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa achukizwa na shambulizi la mabomu mjini Benghazi, Libya



Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amelaani shambulizi la mabomu liliotokea jana mjini Benghazi, Libya na kueleza kushtushwa na uvumi wa kutokea kwa mauaji ya kulipiza kisasi baada ya shambulizi hilo.
Taarifa iliyotolewa na msemaji wa katibu mkuu huyo imesema, Bw. Guterres ametoa salamu za rambirambi kwa wafiwa na kuwatakia majeruhi wapone haraka. Amesisitiza mgogoro wa Libya hautaweza kutatuliwa kwa njia ya kijeshi, na kuongeza kuwa washambuliaji na watu waliolipiza kisasa wote wanapaswa kufikishwa mahakamani.
Habari zinasema, watu 33 wameuawa na wengine 47 kujeruhiwa katika shambulizi hilo, pia video iliyotolewa kwenye mtandao wa internet imeonyesha mwanaume mmoja akiwashambulia kwa risasi watu 10 katika eneo la tukio.

0 comments:

Post a Comment