Mwenyekiti
wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe amefunguka na kulaani vikali kitendo
alichofanya Waziri wa Mambo ya ndani pamoja na Waziri wa TAMISEMI
kumpigia kampeni mgombea wa Ubunge wa CCM jimbo la Siha na kusema kauli
zao zimejaa ubaguzi wa wazi wazi
Mbowe
amesema hayo juzi wakati akizindua kampeni za wagombea wa Ubunge na
udiwani kwa tiketi ya CHADEMA katika jimbo la Siha na kudai Mawaziri hao
wamekuwa wakitumia vibaya madaraka yao.
"Kaja
Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba anawaambia kuwa lazima
mchague CCM, anakuja Jafo Waziri wa TAMISEMI anawaambia wananchi wa Siha
ili mpate maendeleo labda mumchague Mollel, huu ni utoto mtupu.
"Tunapoongozwa
na viongozi wa sampuli hizi, viongozi wabaguzi, viongozi waliopewa
dhamana ya maisha yetu wakafikiri ni mali za baba zao na mama zao
wanakuja kutuambia utoto watu wa Siha tunaakili, kujengwa kwa barabara
si fadhila ya Rais" alisema Mbowe
Mbali
na hilo Mbowe alisema kuwa katika uchaguzi huu wa sasa endapo wataona
gari za Serikali zikitumika kwenye kampeni za wagombea wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM) zitakuwa halali yao.
"Mzee
Mwambigija safari hii kama kufa tufe, safari hii kama noma na iwe noma
tunaomba magari ya Serikali yatumike kwa kazi za Serikali hatutakuwa na
ugomvi lakini magari ya Serikali na vyombo vya Serikali vikitumika
kwenye kampeni za chama chochote ni halali yetu, kwa sababu nchi hii
inaonekana siasa za kistaraabu haziwezekani" alisisitiza Mbowe
0 comments:
Post a Comment