Msanii wa Bongo Fleva, Alikiba jana alipata nafasi ya kumtembelea
mama mzazi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe
Magufuli huko wilayani Chato mkoani Geita.Alikiba ambaye alikuwa Chato jana januari 27 kwa ajili ya show yake
ya ‘Fungua mwaka na King Kiba’ amesema alipata bahati ya pia ya
kutembelea Hospitali ya Chato kwenda kuwaona wagonjwa.
“
leo tuliweza kutembelea HOSPITAL ya wilaya Ya CHATO Kwenda
Kuwaona Wagonjwa Na vile vile tulikwenda Nyumbani Kwa muheshimiwa RAISI
natuliweza kupiga Story Na BIBI yetu MAMA JPM .Nimcheshi Sana na
tulipata baraka zake,“ameandika Alikiba kwenye ukurasa wake wa Instagram.
Tazama picha hapa chini;

Alikiba na timu yake wakiingia katika Hospitali ya wilaya ya Chato

0 comments:
Post a Comment