Monday 29 January 2018

Nchi sita za Afrika zanyakua tuzo ya mapambano dhidi ya Malaria



Nchi sita za Afrika zimepewa tuzo ya kuwa na maendeleo makubwa katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Malaria, wakati bara la Afrika linajitahidi kutimiza lengo la kukomesha Malaria ifikapo mwaka 2030.
Madagascar, Senegal, Gambia na Zimbabwe zimepewa tuzo kutokana na kufanikiwa kupunguza asilimia zaidi 20 ya Malaria kati ya mwaka 2015 hadi mwaka 2016. Algeria na Comoro zimetuzwa kutokana na kukaribia kutimiza mkakati wa kiufundi wa kimataifa GTS uliowekwa na Shirika la Afya duniani WHO na kupunguza Malaria kwa zaidi ya asilimia 40.
Tuzo hizo zimetolewa na muungano wa kupambana na Malaria wa viongozi wa Afrika chini ya mfumo wa mkutano wa 30 wa kilele wa Umoja wa Afrika.

0 comments:

Post a Comment