Sunday 14 January 2018

Ndege ya abiria 168 yanusurika kutumbukia majini

Ndege ya shirika la Pegasus Boeing 737-800 imenusurika kuzama majini baada ya kupoteza muelekeo kwenye uwanja wa ndege nchini Uturuki na kukaribia katika mteremko ulio kando ya bahari.

Ndege hiyo  iliyokuwa na abiria 168, ilikuwa imetoka mjini Ankara na ilitua uwanja wa Trabzon kwenye Black Sea siku ya Jumamosi.
Kila mtu aliyekuwa ndani ya ndege hiyo aliondolewa salama, kwa mujibu wa gavana wa mkoa Yucel Yavuz.
Picha zilionyesha kichwa cha ndege kikiwa chini kwenye mteremko wenye matope mita chache kutoka baharini.
Bw. Yavuz alisema kuwa uwanja huo ulifungwa kwa saa kadhaa wakati uchunguzi ukifanywa.

0 comments:

Post a Comment