Sunday 14 January 2018

Bournemouth yaicharaza Arsenal 2-1

Timu ya Bournemouth yaipa kipindi kigumu Arsenal baada ya kuicaraza mabao 2-1 mbao hayo yalipigwa na kutoka kwa Callum Wilson na Jordon Ibe.

Sasa kikosi cha Arsene Wenge kina mechi tano bila ushindi na kubaki nyumba kwa pointi tano wakati Bournemoutha wakiendelea na mechi nne bila ya kushindwa.
Mlinzi Hector Bellerin aliwapatia wageni waliocheza bila ya Alexis Sanchez, uongozi wakati Alex Iwobi alipomimina kombora kumzidi Asmir Begovic.
Lakini Wilson alitumia fusra ya makosa yake Peter Cech na kutumbukiza mpira wavuni.
Upande wa Eddie Howe ulipata ushindi wa kwanza kabisa dhidi ya Arsenal na kupanda hadi nafasi ya 13 na pointi 4 kutoka hatarini.

0 comments:

Post a Comment