Sunday 28 January 2018

Oprah na Witherspoon wamekuwa gumzo katika jarida la Vanity Fair


Reese Witherspoon amewataka mashabiki wake kumkubali vile alivyo baada ya jarida la urembo la Vanity Fair kuchapisha picha yake akiwa na mguu wa tatu.
Ni miongoni mwa nyota 12 waliopigwa picha na Annie Leibovitz katika chapisho la jarida hilo, ambalo huchapishwa kila mwaka baada ya tamasha la kutoa tuzo.
Vanity fair limejitetea likisema kuwa mguu wa tatu wa Witherspoon ulitokana na rinda alilovaa.


Hatahivyo nyota huyo hakuwa mtu wa pekee kupewa mgu wa tatu .
Katika Picha nyengine iliowekwa katika mtandao wa jarida hilo Oprah Winfrey alionekana kuwa na mkono wa tatu.
Nyota hao wawili walicheka kuhusu ugunduzi huo.


Wakati huohuo, James Franco aliondolewa kwa kutumia njia ya kidijitali katika jarida hilo baada ya kupigwa picha na Leibovitz na kuhojiwa na jarida hilo.
Hii ni baada ya Franco kutuhumiwa na unyanyasaji wa kijinsia na wanawake watano , ikiwemo wanafunzi kutoka shule yake ya uigizaji.
Msemaji alimwambia ripota wa Hollywood: "Tulifanya uamuzi kutomshirikisha James Franco katika piaha ya nje ya jarida hilo baada ya kugundua kuhusu tabia mbaya aliodaiwa kufanya.
Hakuna picha nyengine iliopigwa kwa kuwa wale aliopigwa picha nao walikuwa wamepigwa picha wakiwa kivyao katika makundi mengine.

0 comments:

Post a Comment