Sunday 28 January 2018

MKHITARYAN NA BEGI LA DHAHABU


NA RAPHAEL MWENDA
                 Ukiifuatilia historia wanahistoria wanasema zamani enzi za ukoloni babu zetu walikua wakibadilishana dhahabu kwa tambala la nguo,kioo,miwani na vitu vingine vingi ambavyo thamani yake si ile ya dhahabu ambazo wao walikua wakizitumia kuchezea bao tu.

         Miaka mingi sana imepita toka enzi hizo mpka leo hakuna binadamu anaeweza kufanya biashara ya aina hiyo, jumatatu ya tarehe 21 January ya mwaka 2018 nlipata kushangaa kwa kuona dhahabu ikitoka bila hela katika zama hizi za vyuma kukaza.
       Mnamo mwaka 2016 nikiwa 838kj nilipata taarifa ya kuwa klabu ya Manchester United imemsajili mfalme wa kutengeneza nafasi za kufunga ulaya, anajicho la kutoa pasi za magoli kuliko hata Ozil,Iniesta,verrati na wengineo hakua mwingine bali Henrinkh Mkhtaryan (Armenian Messi). Haikua furaha ndogo kwa upande wa mashabiki wa Manchester United lakini kuna kuruta mmoja aliwahi kunidokeza kwa kusema "Angel Di Maria amefeli ndani ya uzi mwekundu akiwa ametoka kuwa mfalme wa pasi kasi na mchezaji bora wa fainali ya ligi ya mabingwa unaamini Mkhitaryan anaubora kuliko Angel?".
       Jibu lilikua rahisi tu " mfumo wa lui haukumkubali ila huyu kaletwa na Jose" ndio Jose Mourinho alitoa kiasi cha paun 35 kuzileta zile pasi na kasi katika nyasi za old trafford,Mikh alitarajiwa kuja kuwa shetani haswa haswa pale old trafford, lakini sherehe yake iliingia doa mapema tu baada ya msimu kuanza.
         Katika mechi ya Manchester derby alicheza katika kiwango hafifu sana kitu kilichopelekea kutolewa uwanjani baada ya dakika 45 tu, baadae ikaja kujulikana kuwa Mkhi alicheza mchezo ule akiwa na maumivu makali ya goti. Miezi ikapita bila ya muarmenia huyu kutoonekana uwanjani hata pale alipopona hakupewa nafasi kwa kigezo kuwa hana hali nzuri ya kuendana na ligi kuu ya uingereza, lakini aliporudi uwezo wake ulijionyesha dhahiri kwa kuisaidia united kuchukua uropa ligi. Msimu huu pia aliuanza kwa kasi akitoa pasi tano za magoli katika michezo minne ya kwanza si kitu kidogo kufanya hivi katika ligi kuu ya uingereza.

        Miezi sita baada ya mambo haya kutokea Henrikh Mkhitaryan anakwenda Arsenal kwa uhamisho wa kubadilishana wachezaji. Mkhi anakwenda kwa kocha yule yule aliemfanya Thienry Henry kuwa mshambuliaji wa dunia kocha aliemchukua Cesc Fabrigas akiwa mdogo sana kutoka Barca na kumfanya kuwa kiungo yule anaekipiga pale Stanford bridge leo mzee huyu huyu aliemfanya Robin Van Persie kuwa mshabuliaji wa kutisha pale uingereza.Hawa wote walikwenda Arsenal wakiwa wachezaji wa kawaida sana na kuondoka pale wakiwa na majina makubwa.

       Walikua katika mikono salama iliyojaa uvumilivu na kuamini katika kumpa nafasi mchezaji,Arsene Wenger daima anaamini haijalishi kushindwa kufungwa aka kutoa sare,sasa hivi hajapata wale akina Diab,Paulista, na wengineo walioshindwa kuishi katika imani yake sasa hivi kampata Henrikh Mkhitaryan bure kabisa akiwa katika umri usio wa kujifunza tena bali kufanya kazi.

        Namuona Alexander Lacazette akilala na kuamka na tabasamu usoni mwake ndio lazima utabasamu Alexis Sanchez alihitaji kuwa mfalme pale Arsenal kwanini Alexander ufunge kuliko yeye? Sasa ameondoka na mwalimu anakuongezea mtu asiehitaji kufunga sana mtu anaeliogopa goli mwenye aibu na nyavu lakini mwenye miguu ya uchochezi. Kwanini Alexander asifunge ikiwa ana Ozil na mikh nyuma yake? Wote hawa wamezaliwa kumuangalia mshambuliaji kwanini ushindwe kupasia nyavu? 

          Naiona ile dhahabu iliyokua ikichezewa bao pale old trafford ikienda kung'aa ng'ambo imekwenda katika mikono salama mikono inayojua thamani yake na kutambua umuhimu wake katika mchezo wa soka .

0 comments:

Post a Comment