Wizara ya uchukuzi ya Afrika kusini imeanzisha uchunguzi kuhusu ajali
ya treni iliyotokea Alhamisi na kusababisha vifo vya watu 18 na wengine
239 kujeruhiwa. Taarifa iliyotolewa na waziri wa uchukuzi wa Afrika
kusini Bw. Joe Maswanganyi, inasema uchunguzi wa awali unaonesha kuwa
ajali ya treni kuacha reli ilisababishwa na lori lililojaribu kuvuka
reli hiyo saa tatu jana asubuhi wakati treni hiyo inapita, treni hiyo ya
umeme iliwaka moto baada ya kugonga lori na kusababisha vifo na
majeruhi. Waziri Maswanganyi alitembelea eneo la ajali na kutoa salamu
za rambirambi kwa familia za wahanga katika ajali hiyo.
0 comments:
Post a Comment