Kwenye michuano kombe la mataifa
ya Afrika, Sudan imewashangaza wenyeji Morocco kwa kuwalazimisha sare ya
bila kufungana katika mechi yao ya mwisho ya hatua ya makundi jana
mjini Casablanca.
Sudan na Morocco zilizokuwa tayari zimefuzu, ziliingia uwanjani
kusaka timu itakayokuwa vinara wa kundi A baada ya zote kuwa na pointi
zinazolingana, hata hivyo nafasi kubwa ilikuwa kwa Morocco ambao wana
wastani mkubwa wa magoli.
Timu zote zilishambuliana bila ya mafanikio, lakini zaidi fursa ilijitokeza kwa Morocco ambao walizawadiwa penati ambayo golikipa wa Sudan El Hadi Salum aliipangua.
Leo ni zamu ya mechi za kundi B, ambapo timu za Namibia na Zambia zitacheza kutafuta kinara wa kundi baada ya zote kulingana kwa pointi, lakini Uganda na Ivory Coast zitacheza kwa ajili ya kukamilisha ratiba kwa kuwa zote zimekwisha shindwa kufuzu.

0 comments:
Post a Comment