Monday 29 January 2018

Trump amvaa Jay-Z kuhusu maneno yake


Rais Donald Trump amemjibu Jay-Z baada ya mwanamuziki huyo wa muziki wa Rap kumuita "mdudu hatari'' na kumkaripia kwa namna anavyowachukulia watu weusi.
Katika ujumbe wake wa Twitter Bwana Trump alisema kuwa "waMarekani weusi wasio na ajira wameripotiwa kuwa katika viwango vya chini kabisa vya ajira kuwahi kurekodiwa !".

WaMarekani wenye asili ya Afrika wasio na ajira ni asilimia 6.8%, kiwango ambacho ni cha chini kuwahi kurekodiwa.
Lakini wakosoaji wanasema kuwa ukuaji wa uchumi ulianza wakati wa rais Obama na kwamba ukosefu wa ajira miongoni mwao umesalia kuwa wa kiwango cha juu miongoni mwa watu weusi kuliko wazungu.
Alipokuwa katika kipindi cha televisheni ya CNN cha Van Jones Show, Jay-Z alisema kuwa kuangazia viwango vya ukosefu wa ajira ni " kukosa ufahamu wa mambo".
" Sio suala la ukosefu wa pesa pekee lenye umuhimu …pesa haileti furaha... haileti . Hii ni kushindwa kuelewa ukweli . Uwachukulie watu kama binadamu ...hilo ndio suala kuu la muhimu."
Aidha amasesema kuwa kuchaguliwa kwa bwana Trump kulitokana na kushindwa kutatuliwa kikamilifu kwa masuala kadhaa.
"Ukipuliza manukato katika debe la taka ," alisema . " unapofanya hivyo ni nini unafanya pale mdudu hatari anapokuja . unampulizia kitu na hivyo unamfanya mdudu kuwa hatari zaidi kwasababu hujali tatizo ."
" Huchukui taka nje , unaendelea kupuliza dawa juu yake ili kulifanya debe la taka kukubalika. Vitu hivyo vinapokuwa, huwa unabuni mdudu hatari . Na kwa sasa mdudu hatari tulienae ni Donald Trump, mdudu hatari."

0 comments:

Post a Comment