Tuesday 30 January 2018

Umoja wa mataifa walili ongezeko endelevu la uchumi lenye uwiano



Naibu katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Bibi Amina Mohamed ameitaka kamati ya umoja wa mataifa kufanya kazi kuhimiza ongezeko la uchumi lililo shirikishi na lenye uwiano, na kuleta maendeleo endelevu ili kuondoa umaskini.
Akiongea kwenye mkutano wa Baraza la uchumi na mambo ya kijamii la umoja wa mataifa ECOSOC, Bibi Mohamed ameihimiza kamati hiyo kuhakikisha ongezeko hilo linakuwa kamili, kuleta ajira bora na mazingira mazuri ya kazi kwa watu wote, maeneo ambayo amesema kama yakiwa na maendeleo yatachangia kupunguza tofauti katika nchi zinazoendelea.
Bibi Mohamed amesema maendeleo yamepatikana katika kupunguza umaskini, na kutoa fursa za kwenda shule na kupata huduma za afya, kuwawezesha wanawake, vijana, watu wenye ulemavu, wazee na jamii za wazawa. Hata hivyo amesema licha ya mafanikio hayo bado watu hao wanakabiliwa na umaskini.

0 comments:

Post a Comment