Watu
saba akiwemo aliyekuwa fundi wa bomba la mafuta la Tazama, Samwel
Nyakirang'ani (63) wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
wakikabiliwa na mashtaka saba ya uhujumu uchumi kwa kujiunganishia bomba
la mafuta.
Nyakirang'ani
anashtakiwa pamoja na Mwalimu wa Shule ya Msingi ya Ufukoni, Nyangi
Matoro (54), Mfanyabiashara Farijia Ahmed (39), Malaki Mathias (39),
Kristomsi Angelusi(25), Henry Fredrick (38) na fundi ujenzi Pamfili
Nkoronko(40).
Washtakiwa
walisomewa mashtaka yao jana mahakamani hapo na Wakili wa Serikali
Tulumanywa Majigo akisaidiana na Wakili wa Serikali Mkuu Peter Maugo
mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu,Thomas Simba.Wanadaiwa kutenda makosa
yanayowakabili chini ya sheria ya uhujumu uchumi.
Akiwasomea
hati ya mashtaka, Wakili Majigo alidai kuwa kosa la kwanza ni
kujiunganishia isivyo halali katika bomba la mafuta ya Dizeli.
Imedaiwa,
washtakiwa wote katika tarehe tofauti kati ya mwaka 2015 na Januari 8,
mwaka huu, huko maeneo ya Tungi Muungano katika Wilaya ya Kigamboni
jijini Dar es Salaam walijiunganishia bomba la upana wa inchi moja
kwenye bomba la inchi 24 la diesel material yasiyoshika kutu bila kuwa
na kibali cha Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA).
Katika
shtaka jingine la kuharibu miundombinu ( kifaa kinachotumika kwa ajili
ya utoaji huduma muhimu) imedaiwa katika tarehe na maeneo hayo hayo,
washtakiwa kwa pamoja walitoboa na kuharibu bomba la Inchi 24
linalotumika kusambaza mafuta ya Dizeli mali ya TPA.
Washtakiwa
hao wanadaiwa pia kuwa, kati ya 2015 na January 8, 2018 maeneo ya Tungi
Kigamboni, walitoboa bomba la inchi 28 la mafuta linalotumika kwa ajili
ya usambazaji wa Crude Oil likiwa ni mali ya TPA.
Baada
ya kusomewa mashtaka hayo, Wakili Majigo alidai Mkurugenzi wa Mashtaka
(DPP) amewasilisha hati ya kuzuia dhamana kwa washtakiwa hao.
Washtakiwa
hawaruhusiwi kujibu lolote kwa kuwa kesi inayowakabili ni ya uhujumu
Uchumi ma imeahirishwa hadi Januari 30,2018. Kwa mujibu wa upande wa
mashtaka, upelelezi bado haujakamilika, washtakiwa walirudishwa rumande.
0 comments:
Post a Comment