Tuesday 27 February 2018

Kombe la Dunia latua Kenya



Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta akiwa na Kombe la Dunia la Fifa ikulu jijini Nairobi leo.
Kombe hilo linatembezwa mataifa mbalimbali kabla ya michuano ya Kombe la Dunia kuanza Juni nchini Urusi.
Ni mara ya tatu kwa kombe hilo kuwa Kenya, awali ikiwa 2010 na 2013 katika ya fainali zilizofanyika Afrika Kusini na Brazil.

Kenya ni ya 21 mwaka huu kuwa mwenyeji wa kombe hilo mwaka huu kati ya mataifa 51 yanayotarajiwa kulipokea kabla ya Juni.
Kesho, Wakenya wana fursa ya kulitazama na kupigwa picha KICC kabla ya kombe hilo kuelekea Maputo, Msumbiji.

0 comments:

Post a Comment