Tuesday 27 February 2018

Miguna ruksa kurejea Kenya



Mahakama Kuu imetoa amri kwa Maafisa Uhamiaji nchini humo kumruhusu Mwanachama wa Upinzani kurejea nchini baada ya kuondolewa kwa nguvu mapema mwezi Januari 2018

Jaji wa Mahakama hiyo Chacha Mwita ameiamuru idara ya Uhamiaji kumpa Miguna hati zake za kusafiria ili kumwezesha kurejea mpaka hapo shauri lake litakaposikilizwa juu ya uhalali wa uraia wake
Amri kama hii ilishatolewa awali na Mahakama hii lakini Serikali ilisema haiwezi kufanya hivyo kwa maana Miguna sio raia wa Kenya

Miguna Miguna ambaye ni mwanachama wa Muungano wa upinzani NASA na pia ni Wakili alilazimishwa kupanda ndege na kurudishwa nchini Canada

Kufukuzwa huko nchini kulifuatia kukamatwa kwake na kufunguliwa mashtaka ya uhaini kwa kuhusika na zoezi la kujiapisha kiongozi wa upinzani Raila Odinga

0 comments:

Post a Comment