Thursday 1 February 2018

TANZIA-Msanii mkongwe nchini Uganda Moozey Radio afariki dunia


 Mwanamuziki mkongwe kutoka nchini Uganda, Moses Sekibooga maarufu kwa jina la kisanii Mozey Radio afariki Dunia leo katika hospitali ya Mulago jijini Kampala.

Kifo cha Msanii huyo kimekuja siku moja baada ya Rais Yoweri Museveni kuchangia Shilingi Milioni 30 za Uganda kwaajili ya matibabu na pia matayarisho ya misa ya kumuombea katika kanisa lililopo maeneo ya Nansana siku ya Jumapili.

Wiki iliyopita Mwanamuziki huyo alivunjika shingo na fuvu la kichwa baada ya kuanguka wakati akigombana na Mlinzi wa ukumbi mmoja wa starehe jijini Kampala.

0 comments:

Post a Comment