Monday 26 March 2018

Grace Mugabe ndani ya tuhuma nzito



Polisi wameanza kumchunguza Grace Mugabe juu ya madai ya kuongoza mtandao wa kijangili na usafirishaji haramu wa pembe za ndovu.
 
Grace ambaye ni Mke wa Rais wa zamani wa nchi hiyo, Robert Mugabe pia anatuhumiwa kusafirisha almasi na dhahabu kutoka nchini humo kinyume cha sheria.


Rais wa sasa wa nchi hiyo, Emmerson Mnangagwa, aliagiza uchunguzi wa dharura katika shughuli za Bi. Grace baada ya ushahidi wa 'nguvu sana' uliotolewa na Adrian Steirn, mwandishi wa picha wa Australia.

0 comments:

Post a Comment