Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) leo Machi 25, imemteua Athuman Nyamlani kukaimu nafasi Makamu wa rais wa shirikisho hilo
Nyamlani ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, ameteuliwa kushika nafasi hiyo baada ya Michael Wambura kufungiwa maisha kujihusisha na soka
Wambura amefungiwa na kamati ya maadili ambayo imeeleza kumtia hatiani na makosa kadhaa yakiwemo ya kugushi nyaraka kwa ajili ya malipo ambayo yameelezwa hayakuwa sahihi
0 comments:
Post a Comment