Friday 2 March 2018

Jay-Z aongoza kwa mkwanja mrefu


.



Rapper Jay-Z utajiri wake unakaribia kufikia thamani ya Dollar Billion 1 (Tshs Tirion 2) na atakua msanii wa kwanza wa Hip Hop kufikia kiasi icho.

Kwa mujibu wa jarida la #Forbes wametoa orodha ya wasanii wa Hip Hop wenye mkwanja mrefu duniani na nafasi ya kwanza imeenda kwa Jay-Z mwenye Thamani ya dollar million 900 sawa na Shilingi Tirioni 1.8 za Tanzania. Jay-Z ameingiza pesa hizo kupitia label yake ya #rocnation , #Tidal na kinywaji chake cha Armand De Brignac.
 
Nafasi ya pili imeenda kwa P Diddy akiwa na $825 million ambazo ameingiza kupitia vinjwaji vyake vya Ciroc Vodka, DeLeon Tequila brand, pamoja na matangazo ya television yake ya Revolt TV.
Nafasi ya tatu imeenda kwa producer Dr Dre akiwa na mkwanja wa $770 million, huku nafasi ya 4 na 5 zikienda kwa #Drake na #Eminem wakilingana kwa mkwanja wa dollar million 100.


0 comments:

Post a Comment