Saturday 24 March 2018

Kesi ya Babu Seya yafikia ukingoni



Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu, imesema Mahakama za Tanzania zilitenda haki na kukiuka pia kwa upande mwingine katika hukumu ya Babu Seya na Papii Kocha.
Mahakama imewaruhusu Babu Seya pamoja na Papii Kocha kuwasilisha hoja ya kuomba fidia kulingana na haki zao ziliokiukwa


Mfano wa haki iliyokiukwa ni kukaaa mahabusu kwa siku 4 bila kufahamishwa makosa yao lakini pia hawakuwa na wakili wa kuwatetea


Pia wawili hao waliomba kupimwa mkojo na damu ili kuthibitishwa kama waliwaingilia Watoto wale ambao upande wa Jamhuri ulidai waliambukizwa magonjwa ya zinaa lakini walikataliwa


Maombi hayo yanapaswa kuwasilishwa ndani ya kipindi cha siku 30

0 comments:

Post a Comment