Tuesday 13 March 2018

Maria Sarungi kumpeleka mahakamani Musiba



Mwanaharakati na mwanamitindo maarufu Maria Sarungi afungua kesi ya madai dhidi ya Mhariri wa gazeti la Tanzanite, Cyprian Musiba kwa kumchafua na kumkashifu mbele ya Wanahabari tarehe 25 Februari 2018

Musiba aliwataja Maria Sarungi pamoja na Maxence Melo, Evarist Chahali, Freeman Mbowe, John Heche, Mange Kimambi, Tundu Lissu, Godbless Lema, Julius Mtatiro na Zitto Kabwe kama watu hatari kwa usalama wa nchi katika orodha hiyo ya watu 10.

Kabla ya kufungua shauri hili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Maria alimtaka ndugu Musiba pamoja na Mkurugenzi wa gazeti la Tanzanite kuomba radhi ndani ya siku 7 lakini kwasababu zisizofahamika bwana Cyprian Musiba hakufanya hivyo

Aidha katika taarifa iliyotolewa na Wakili Benedict Ishabakaki imeeleza kuwa waendeshaji wa ukurasa wa Dar24 katika mitandao ya kijamii nao pia walitakiwa kufuta taarifa hiyo pamoja na kuomba radhi lakini licha ya kufuta taarifa ya kumchafua mteja wake bado wanasubiriwa waombe radhi la si hivyo watawaunganisha katika shauri hili

0 comments:

Post a Comment