Tuesday 27 March 2018

Mfanyabiashara wa madwa ya kulevya adaiwa kutaka kutoa rushwa



Mfanyabiashara wa Dawa za Kulevya Adaiwa kutaka kumhonga shilingi bilioni 1 Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ili asikamatwe.

 Kamishna Sianga amesema kuwa Mfanyabiashara huyo wa kemikali bashirifu ambaye hakumtaja jina alitaka kumpa rushwa ya shilingi milioni 400 Kamishna wa Sheria wa Mamlaka hiyo ili aharibu kesi ili asishtakiwe.


Kamishna Sianga alisema pamoja na jitihada za kutaka kuhonga, kigogo huyo na mwenzake walikamatwa mkoani Mwanza.


Alibainisha kuwa waliokamatwa katika usafirishaji wa kemikali hizo ni Mwita Ikohi na Chola Maginga ambao tayari wamefikishwa mahakamani.

0 comments:

Post a Comment