Tuesday 27 March 2018

Johana Konta afuzu raundi ya nne


Mwanadada Johana Konta wa Uingereza amefanikiwa kufuzu raundi ya nne ya mashindano ya tennis ya Miami nchini Marekani baada ya kumshinda Elise Mertens wa Ubelgiji kwa seti ya mbili sifuri yenye alama 6-2 6-1.
Katika raundi ya nne, Konta ambaye ni bingwa mtetezi wa mashindano hayo, atakutana na mchezaji namba nane kwa viwango vya ubora duniani Venus Williams ambaye amefuzu baada ya kumfunga Kiki Bertens wa Uholanzi.

0 comments:

Post a Comment