Sunday 25 March 2018

Mkwasa awavaa Taifa Stars adai wanachelewa sana kuchukua maamuzi



 Kocha Mkuu wa zamani wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa amesema wachezaji wa Tanzania wanafungwa mechi ngumu kwa sababu ni wazito wa kufanya maamuzi binafsi wanapokuwa uwanjani

Mkwasa ameeleza kuwa tatizo kubwa la wachezaji wa Tanzania ni kutegemea zaidi maelekezo kutoka kwa kocha badala ya uwezo wao wenyewe, hivyo huishia kufanya vibaya kwenye michezo muhimu

Akizungumzia michezo ya kimataifa ya siku za hivi karibuni, Mkwasa amesema Taifa Stars ilipoteza kizembe mchezo wa kirafiki dhidi ya Algeria, ambapo ilifungwa mabao 4-1

Kocha huyo ambaye miaka 2 iliyopita alikuwa akiifundisha Taifa Stars, ametoa wito kwa timu ya Taifa kujiandaa vyema kwa ajili ya mchezo mwingine dhidi ya DRC, utakaochezwa mnamo Machi 27 jijini Dar es Salaam ili kuepuka kurudia makosa.

0 comments:

Post a Comment