Wednesday 7 March 2018

Mo Farah azidi kuwa 'Moto'marathon London



Mwingereza Mo Farah alimshinda Mkenya Daniel Wanjiru na kushinda mzunguko wa kwanza wa mbio za nusu marathoni za London, huku Callum Hawkins akimaliza katika nafasi ya tatu. Bingwa huyo mara nne wa Olimpiki alishiriki kwenye mbio hizo za nusu marathoni kujiandaa kwa mbio za marathoni za London zitakazoandaliwa mwezi Aprili. Farah mwenye umri wa miaka 34 ananuia kuwa mwanariadha wa kwanza wa Uingereza kushinda mbio za wanaume tangu mwaka 1993.

0 comments:

Post a Comment