Wednesday 7 March 2018

Simba SC kuwavaa wamisri Al Masry Taifa


Wekundu wa Msimbazi Simba SC leo majira ya saa 12:00 jioni saa za Afrika Mashariki, itakutana na Al Masry ya Misri katika mchezo wa kwanza wa raundi ya kwanza ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Mchezo huo utapigwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Timu hizo zitarudiana baada ya siku 10 mjini Cairo Misri, mshindi ataingia kwenye mchujo wa kuwania kuingia hatua ya makundi.
Kocha wa Simba Pierre  jana katika ukumbi wa TFF amesema kuwa anatumaini  timu yake itashinda.

0 comments:

Post a Comment