Monday 5 March 2018

Msikiti uliotakwa kubomolewa sasa wapewa kibali kujengwa



Rais Magufuli ametoa kibali cha kuendelea kujenga msikiti mkoani Rukwa(ambao awali ulizuiliwa) hadi umalizike

Amesema amefikiria mambo mengi mpaka kufikia maamuzi hayo ikiwemo kuleta muskabali wa maridhiano, amani, utulivu, mshikamano na maelewano kwa wana Rukwa na amesema yupo tayari kuuzindua

Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Rashid Akilimali amesifu maamuzi ya Rais na kulikubali ombi lake la kutaka kuja kuweka jiwe la msingi ama kuuzindua msikiti huo na kuwa waislamu wataendelea kuungana nae na kumuombea amalize vipindi vyake salama

Uongozi wa Serikali ya Mkoa wa Rukwa ukiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo, Joachim Wangabo umetoa mchango wa Shilingi 5,700,000/- ikiwa ni ahadi na fedha taslim.

0 comments:

Post a Comment