Friday 9 March 2018

Rais Kenyatta,Odinga mambo shwari



Rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa NASA Raila Odinga wanakutana na kufanya mazungumzo katika jengo la ‘Harambee House’ huko Nairobi.

Lengo la mazungumzo hayo bado halijajulikana lakini viongozi wawili hao wanatarajiwa kufanya mkutano na vyombo vya habari muda wowote kuanzia sasa

Ikulu ya Kenya ilitangaza kuwa Rais Kenyatta ataongea na vyombo vya habari majira ya saa 5 asubuhi ya leo

Awali, Kumekuwa na wito wa majadiliano kutoka Marekani na nchi nyingine baada ya Raila Odinga kukataa kukubali Uhuru Kenyatta kama rais halali


Raila Odinga amesema yeye pamoja na ndugu yake Uhuru Kenyatta wamekubaliana kuwa mgawanyiko ulikuwepo toka enzi za uhuru unaisha tangu leo.
Kwa upande wa Uhuru Kenyatta amesema taifa la Kenya ni kubwa kuliko mtu yeyote, hivyo lazima viongozi waungane ili wananchi na taifa kwa ujumla liungane

Makubaliano hayo ya viongozi hao wawili yamekuja baada ya kufanya mazungumzo leo asubuhi Machi 9, 2018 katika jengo la Harambee House

0 comments:

Post a Comment