Friday 9 March 2018

Zanzibar kujenga kiwanda cha kutengeneza simu



Zanzibar inatarajia kujenga Kiwanda cha kuunganisha na kutengeneza simu za mkononi na kutoa ajira kwa wananchi visiwani humo

Kiwanda hicho kitakachoanzishwa hivi karibuni na Kampuni ya USI kutoka Korea Kusini, kitaanza kwa kuunganisha vifaa vya simu na kisha baada ya miaka minne kuanza kutengeneza simu
Mkuu wa mkoa wa Mjini Magharibi, Ayoub Mahmoud alisema wiki mbili zilizopita wamesaini makubaliano na Kiwanda cha simu za mkononi na tayari wawekezaji hao wamepewa eneo katika eneo la viwanda vidogo

Aidha, ameongeza kuwa kwa sasa wanamalizia taratibu na katika miezi miwili hadi mitatu watakuwa wameanza kazi ya kuunganisha simu kutoka Korea Kusini

0 comments:

Post a Comment