Friday 9 March 2018

SUMATRA Kugawanywa,waziri afafanua



Serikali inatarajia kuigawa Mamlaka ya Usafirishaji Majini na Nchi Kavu (SUMATRA), ili kupata taasisi ambayo itashughulikia suala la usafiri wa majini na nyingine nchi kavu

Hayo yalibainishwa jana Machi 7 na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, alipokuwa akifungua Baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa

Prof. Mbarawa alisema kuna fedha nyingi ambazo bado hawajaweza kuzipata, walishajaribu kuigawa Mamlaka lakini ilishindikana. Anaamini safari hii itawezekana

Aidha, alisema Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA), itanunua rada nne zitakazo gharimu Sh. bilioni 63. Fedha hizo 50% inategemea mapato ya ndani ya taasisi hiyo na zinazobaki zinatoka Serikalini.

0 comments:

Post a Comment