Tuesday 3 April 2018

Boko Haram waua watu 18




 Takriban watu 18  nchini Nigeria wameuawa na wengine 86 kujeruhiwa katika shambulizi lililofanywa na waasi wa Boko Haram

Waasi hao waliokuwa wakipambana na wanajeshi wa Serikali karibu na kaskazini mashariki mwa Maiduguri usiku wa kuamkia leo

Watu waliouawa wanatoka katika vijiji viwili vya Bale Shuwa na Bale Kura vilivyoko Maiduguri

Maiduguri mji mkuu wa jimbo la Borno ndiyo chimbuko la kundi hilo la waasi la Boko Haram lililoanza uasi miaka 9 iliyopita kaskazini mashariki mwa Nigeria.

0 comments:

Post a Comment