Sunday 1 April 2018

Prof Mkumbo amtumia barua Askofu mkuu KKKT



Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Prof. Kitila Mkumbo amejibu Waraka wa Pasaka kutoka kwa Maaskofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) ulioeleza kuhusu matukio ya kupotezwa kwa watu na kubanwa kwa demokrasia nchini

Katika ujumbe wake, Prof. Kitila amesema ni hatari kwa Kanisa kutoa kauli inayosababisha maumivu na mifarakano katika nchi badala ya kuponya

Prof. Kitila ambaye ni muumini wa KKKT, amesema anakubaliana na mengi maaskofu waliyogusia katika Waraka huo. Hata hivyo, amelitahadharisha kanisa kujiepusha na kuonekana lipo upande fulani katika mijadala ya kitaifa hususan ile inayoigusa jamii moja kwa moja

Amesisitiza kuwa ni muhimu kwa kanisa kupima kwa umakini mkubwa uzito wa kila neno kabla ya kutoa kauli kwa umma.

Waraka wa Maaskofu 27 wa KKKT ulitoka hivi karibuni na kusomwa katika Makanisa yote ya Kilutheri Machi 25, 2018 ambapo kupitia waraka huo walizungumzia masuala ya Uchumi, Katiba Mpya, Siasa na Jamii kwa ujumla.

0 comments:

Post a Comment