Sunday 1 April 2018

Naibu waziri wa Afya atoa ufafanuzi juu ya mama aliyezaa mapacha waume tofaiti



Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Faustine Ndugulile amefafanua uwezekano wa kisayansi kwa mwanamke mmoja kubeba ujauzito mapacha kutoka kwa wanaume wawili tofauti

Amesema jambo hilo hutokea pale mwanamke anapotoa mayai mawili tofauti katika mzunguko mmoja ambayo yanaweza kurutubishwa (fertilized) na mbegu za wanaume 2 tofauti. Kisayansi inaitwa Super-fecundation.

Ndugulile ambaye ni daktari kitaaluma, ametoa ufafanuzi huo kutokana na habari kuhusu mwanamke mmoja nchini Uganda kuingia kwenye mgogoro wa kindoa na mumewe, baada ya wanaume wawili (mumewe na mdogo wake) kujikuta wote wawili ni baba wazazi halali wa watoto wawili mapacha, kila mmoja akiwa na mtoto mmoja baada ya kupimwa DNA.

"Kisayansi inawezekana. Inatokea pale mwanamke anatoa mayai mawili tofauti katika mzunguko huo mmoja ambayo yanakuwa-fertilized na mbegu za wanaume wawili tofauti. Kisayansi inaitwa superfecundation" ameeleza Dkt. Ndugulile kupitia ukurasa wake wa Twitter.

0 comments:

Post a Comment