Wednesday 30 May 2018

Mwanafamili ya Whitney Houston amtetea Kanye West





Mwanafamilia mmoja wa familia ya Whitney Houston amkingia kifua Kanye West, asemwa wa kulaumiwa ni aliyepiga picha

Ijumaa hii rapper Pusha T aliachia album mpya “Daytona” na ukiachana na diss ya Drake kitu kingine kilichoongelewa sana kutoka kwenye hii album ni cover yake

Cover ya hiyo album ilipigwa mwaka 2006 kwenye chumba cha Whitney Houston kipindi alikuwa kwenye steji mbaya ya matumizi ya dawa za kulevya

Watu wengi wameikosoa cover hiyo ikiwemo ndugu wa Whitney Houston ambao wanataka Kanye West iabadilishe hiyo cover na kuwaomba msamaha mara moja

Gary Michael, moja ya ndugu wa Whitney Houston ameibuka na kumtetea Kanye West aliyelipa Million 193 Tsh kupata haki za kuitumia picha hiyo, Gary amesema Kanye hatakiwi kulaumiwa bali mtu ambaye aliipiga hiyo picha -
Amesema mtu aliyeipiga hiyo picha na kuiuza ndio mbaya zaidi kwa hiyo familia kuliko Kanye West

0 comments:

Post a Comment