Thursday 31 May 2018

Mwandishi apigwa risasi Ukraine



Mwandishi wa habari wa Urusi, Arkady Babchenko(41) aliyekuwa mkosoaji mkubwa wa vile alivyodai ni vitendo vya uchokozi vinavyofanywa na Urusi nchini Georgia, Crimea, Mashariki mwa Ukraine na Syria, ameuawa kwa kupigwa risasi.
  • Babchenko alifariki dunia Jumanne wakati akipelekwa hospitali baada ya mke wake kumkuta chumbani akivuja damu. Polisi nchini humo wamefungua jalada la uchunguzi huku wakihusisha kifo chake na masuala aliyokuwa akiyafanyia kazi
    -
    Aidha, Ukraine imeishutumu Urusi kwa kuhusika na mauaji hayo huku Urusi ikipinga vikali shutuma hizo kwa Waziri wake wa Mambo ya Nje, Sergei Lavrov kusema "Ni kitu kibaya sana Urusi kuhusishwa na Mauaji ya Mwandishi wa habari"
    -
    Mwandishi huyo aliondoka Urusi mwaka 2017, akikabiliwa na vitisho vya kupokonywa uraia wake na kuongezeka kwa vitisho dhidi yake kutokana na maoni yake kuhusu ajali ya ndege ya Desemba 2016
    -
    Ajali hiyo ya ndege iliwauwa waimbaji wa kwaya ya Jeshi la Urusi waliokuwa njiani kwenda Syria kuwatumbuiza marubani wa Jeshi

    0 comments:

    Post a Comment