Thursday 31 May 2018

Kocha anayepanga matokeo Saudi Arabia afungiwa maisha



Shirikisho la Mpira wa Miguu Dunia, FIFA limemuondoa Refa Fahad Al-Mirdasi na timu nzima ya Marefa kutoka nchini ya Saudi Arabian katika orodha ya Marefa watakaochezesha mechi za Kombe la Dunia nchini Urusi mwaka huu

FIFA imefikia uamuzi huo baada ya refa Al-Mirdasi kufungiwa maisha kujihusisha na masuala ya mpira nchini Saudi Arabia kutokana na kujihusisha na upangaji wa matokeo ya mechi. Inasemekana aliomba fedha kutoka kwa timu moja ili kuisaidia kushinda mchezo wa fainali

Refa huyo, Fahad Al-Mirdasi ametoa kadi nyingi nyekundu kwa muda ambao amekuwa akichezesha mechi nchini Saudi Arabia

Marefa wawili kutoka Japan na Umoja wa nchi za Kiarabu Emirate ndio wataenda kwenye michuano hiyo ya Kombe la Dunia kama mbadala wa timu ya Marefa kutoka Saudi Arabia

0 comments:

Post a Comment