Monday 11 June 2018

21 Savage afanya maamuzi ya kutokuvaa cheni



Inaweza kuwa ni habari mbaya kwa kampuni zinazojishughulisha na uuzaji wa vitu vya thamani kama cheni kutokana na kauli ya mwanamuziki 21 Savage ya kusema kuwa ameacha rasmi kuvaa vito vya thamani shingoni mwake.

21Savage akizungumza na jarida maarufu la Forbes amesema kuwa amekuwa akipoteza fedha nyingi katika kununua vitu vya gharama hasa cheni kitu ambacho ametokea kuchukizwa nacho kwani muda wa vitu hivyo kuonekana kuitw na wakati kwa upande wake.


"Ninaacha kuvaa vito vya thamani kwasababu kila mtu huvaa na kuwakosea adabu wasiovaa. Niliiacha; Ninapata busara kidogo na kukua hivyo ... Sababu nyingine ni kwa sababu watu matajiri ambao nimewahi kukutana nao katika maisha yangu,sijawahi kuwaona wakiwa wamevalia vito hivyo,"amesema 21 Savage.

Unaweza kuangalia mahojiano ya Vogue ya 21, ambayo pia huzungumzia umuhimu wa mtindo, Itazame Chini.




0 comments:

Post a Comment