Wednesday 6 June 2018

Kuna safari ndefu Rais wa Marekani na Urusi kukutana



Balozi wa Marekani nchini Urusi amesema kuwa kuna njia ndefu sana kabla ya Marais Vladmir Putin wa Urusi na Donald Trump wa Marekani kuweza kukutana.

Jon Huntsman Jr. ameyasema hayo wakati akifanya mahojiano ya televisheni na kuongeza kuwa, ikiwa kutahitajika marais wa Marekani na Urusi kukutana, basi kwanza itatangazwa na Rais Trump kuhusiana na muda na mahala kutakapofanyika kikao hicho.

Matamshi ya balozi huyo wa Marekani nchini Urusi yametolewa katika hali ambayo kabla ya hapo kuliripotiwa kwamba viongozi wa White House wanafanya maandalizi kwa ajili ya kikao kati ya Rais Donald Trump na Vladmir Putin huku Trump pia akiwa ametangaza kuwa yupo tayari kwa ajili ya kukutana na rais huyo wa Urusi.

0 comments:

Post a Comment