Thursday 7 June 2018

TANZIA: Sam wa Ukweli aaga Dunia



Msanii wa Bongo Fleva, Salum Mohamed maarufu 'Sam wa Ukweli' amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Juni 07 katika hospitali ya Palestina, Sinza baada ya kuugua kwa muda mrefu

Taarifa za awali kutoka kwa Mtayarishaji wa nyimbo zake aliyefahamika kwa jina la Steve zinasema Sam alianza kulalamika maumivu ya tumbo tangu Jumanne Juni 05 hadi kuzidiwa Jumatano usiku

Aidha, Sam alionekana kusumbuliwa na tumbo hilo kwa muda mrefu maana lilipoanza kumuuma alidai huwa anakunywa vitu vya moto na anapona, hivyo Steve na wenzake walifanya harakati za kumtafutia ama Mtori au supu

Kwa sasa Mwili wa Mwanamuziki Sam wa Ukweli umehifadhiwa katika hospitali ya Mwananyamala

0 comments:

Post a Comment