Wednesday 13 June 2018

Victoria na Beckham wadaiwa kuachana


Staa wa maswala ya mitindo Victoria Beckham adaiwa kuachana na mume wake David Beckham, hayo yamekuja baada ya kuonekana Siku tatu mfululizo bila Pete ya ndoa.

Kwa mujibu wa mtandao wa Mirror kutoka nchini Marekani,wamedai kuwa jambo la Victoria kutoonekana na Pete ya ndoa halijazoeleka kwa wawili hao.

Wawili hao katika maisha yao ya ndoa wamefanikiwa kupata watoto wanne ambao ni Brooklyn, Harper Seven, Romeo pamoja na Cruz.

0 comments:

Post a Comment