Monday 30 July 2018

Bondia Dillian Whyt azidi kuonesha ubabe kwa Joseph Paker


Pambano lililofanyika katika viwanja vya Cardiff nchini Wales, huku bondia Dillian Whyte wa Uingereza alifanikiwa kupata ushindi kwa njia ya pointi dhidi ya mpinzani wake Joseph Parker wa New Zealand.
Whyte alishinda kwa wingi wa pointi, kulingana na majaji akipata 113-112, 115-110, 114-111, na bondia huyo kwa sasa anatazamiwa kuanza maandalizi ya kuwania mikanda ya uzito wa juu dhidi ya Deontay Wilder wa Marekani au Anthony Joshua wa Uingereza.
Kwa upande wa mapambano ya Utangulizi, mwanadada Katie Taylor kutoka Ireland ya Kaskazini alimshinda Kimberley Connor wa Marekani kwa KO katika raundi ya tatu, na bondia huyo sasa amefanikiwa kutetea mataji yake ya ubingwa wa IBF na WBA.

0 comments:

Post a Comment