Tuesday 31 July 2018

Qatar yakataa kutumia rushwa kuruhusiwa kombe la dunia 2022


Shirikisho la soka nchini Qatar limepinga vikali madai yote yaliyowasilishwa FIFA kuwa ilitumia rushwa ili kupata nafasi ya kuwa mwenyeji wa michuano ya kombe la dunia mwaka 2022.
Qatar imefafanua hayo baada ya gazeti moja la nchini Uingereza kuitaka FIFA ifanye uchunguzi dhidi ya njia zilizotumika mwaka 2010 kuipatia nchi hiyo uenyeji wa michuano ya kombe la dunia mwaka 2022.
Katika madai yaliyofikishwa FIFA, inasemekana kuwa Qatar ilitoa rushwa na kuunda kikosi-kazi kwa ajili ya kufanya njama za kuwafuta wapinzani wakati wa kinyang'anyiro cha kuwa wenyeji wa michuano ya kombe la dunia mwaka 2022.
Wapinzani wa karibu wa Qatar kwa wakati huo walikuwa ni Marekani, Australia, Korea Kusini na Japan.

0 comments:

Post a Comment