Jeshi la nchi hiyo limeitungua ndege ya kivita ya Syria baada ya kuingia katika anga la Israel leo mchana Julai 24 na kuongeza hofu zaidi ya mapigano ya kijeshi katika eneo hilo
Kwa mujibu wa Jeshi la Israel, ndege hiyo iliyotengenezwa nchini Urusi iliingia kilometa mbili katika anga la Israel na makombora mawili yalitumwa kuizuia
Katika tukio hilo inadaiwa kuwa rubani wa ndege hiyo alifariki
Hata hivyo, Syria imesema kuwa ndege hiyo ilikuwa inaendesha uchunguzi dhidi ya makundi ya kigaidi
September 2014, Israel ililipua ndege ya kivita ya Syria iliyokuwa imeingia kilometa moja katika anga la Israel, marubani wote wawili walifanikiwa kutoka na kutua Syria

0 comments:
Post a Comment