Meneja wa Manchester United,
Jose Mourinho, amelazimika kukatisha likizo ya beki wake Ashley Young na
kumtaka kurudi kwenda kusaidia safu ya ulinzi ya klabu hiyo kufuatia
matokeo yasiyoridhisha katika mechi za maandalizi. Mourinho amezungumza
hayo baada ya mchezo wa International Championship Cup (ICC) wa
Manchester United na AC Milan uliopigwa nchini Singapore ambapo katika
mchezo huo, United ilishinda kwa penalti 9-8 baada ya kutoka sare ya
1-1. Pia kocha Jose Mourinho amethibitisha kuwa atamruhusu Matteo
Darmian kuondoka klabuni hapo watakapopata ofa ambayo wataridhika nayo.
Manchester United inakosa huduma ya wachezaji wake muhimu katika safari
yake ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi, wachezaji ambao bado wako
likizo ni Ashley Young, David de Gea na Romelo Lukaku.

0 comments:
Post a Comment