Mwanamuziki maarufu wa muziki wa dansi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Koffi Olomide azuiwa kuingia nchini Zambia kutokana na tuhuma za kumdhalilisha Mwanahabari nchini humo
Koffi Olomide anatuhumiwa kwa makosa ya utovu wa nidhamu alioufanya kwenye nchi ya Afrika Kusini na Ufaransa
Serikali ya Zambia imemwambia mwanamuziki huyo kuwa itamkamata endapo atawasili nchini humo
Koffi pia anatuhumiwa kuwadhalilisha wanenguaji wake, kuwashikilia kama mateka na kuwafanyisha kazi kinyume cha utaratibu nchini Ufaransa.
Mwanamuziki huyo amewaomba radhi wananchi wa Zambia na kuongeza kuwa anawapenda Wanawake wa Zambia na anaihesabu nchi hiyo kama nyumbani kwao
0 comments:
Post a Comment