Tuesday 31 July 2018

Lebron James afungua shule jimboni kwake



Mchezaji wa Kikapu kutoka timu ya Lakers,nchini Marekani Lebron James @kingjames amezindua rasmi shule kutoka katika taasisi yake Jame's Foundation huku dhumuni ya shule hiyo ni kusaidia wale wenye vipaji maalumu na uwezo Mdogo wa kifedha.

Shule hiyo iitwayo 'I Promise School' imejengwa katika sehemu ambayo @kingjames amezaliwa katika jimbo la Ohio.

Ikumbukwe kuwa Lebron James amekuwa mstari wa mbele katika kuibua vipaji mbalimbali na hii ni kutokana na mipango ndani ya taasisi yake ya James Foundation.

Rapa Meek Mill amempongeza mwanamichezo huyo kwa kuwa mfano mzuri katika jamii.
.

0 comments:

Post a Comment