Tuesday 31 July 2018

Fury Athibitsha kuzichapa na Deontray Wilder Disemba mwaka huu


Bondia Tyson Fury wa Uingereza amethibitisha kupitia ukurasa wake wa twitter kwamba mazungumzo kwa ajili ya pambano dhidi ya Deontay Wilder wa Marekani linalotazamiwa kufanyika mwezi Disemba mwaka huu yanaendelea vizuri.
Katika ujumbe wake huo, Fury amesema analihitaji pambano hilo ili kurejesha ubingwa wake wa WBC ambao alipokwa miaka mitatu iliyopita.
Tangu arejee kwenye masumbwi baada ya kukosekana kwa muda mrefu kutokana na kifungo, Fury ameshiriki na kushinda pambano moja dhidi ya Sefer Seferi wa Albania mwezi Juni na anatarajiwa kupigana na Fancesco Pianeta wa Italia Agosti 18.

0 comments:

Post a Comment