Thursday, 26 July 2018

Martial aondoka kikosini



Anthony Martial ameondoka katika Kambi ya Manchester United nchini Marekani na kurejea Jijini Manchester ili kuwa Karibu na Mpenzi wake Melanie anayetarajia kujifungua Mtoto wa Kiume hivi karibuni.

Mchezaji huyo amepewa ruhusa na Kocha wake Jose Mourinho ingawa kitendo cha Mshambuliaji huyo kuondoka Kambini kinazidi kufanya Kikosi cha Man U kuwa na Wachezaji wachache kutoka Timu ya Wakubwa.

Martial amekuwa akihusishwa kuondoka Klabuni hapo huku Vilabu vya Chelsea na Bayen Munich vikihitaji huduma ya Mshambuliaji huyo.

0 comments:

Post a Comment