Friday 3 August 2018

Facebook na Instagram kuja na mpangoo


Mitandao ya Facebook na Instagram inazindua programu mpya itakayodhibiti muda unaotumiwa na wateja wao katika mitandao hiyo

Programu hiyo itapatikana katika ukurasa wa 'settings' katika mitandao yote miwili baada ya kubofya 'Your Activity' katika Instagram ama 'Your Time katika Facebook'

Hatua hii inakuja kufuatia malalamiko kwamba utumiaji wa muda mrefu unaweza kuathiri vibaya afya ya akili

Aidha, watumiaji sasa wataweza kuona kiwango cha muda waliotumia katika mitandao hiyo miwili na kujikumbusha muda waliofikia ili kufunga ujumbe wanaopata kwa muda fulani

Facebook ilichapisha chapisho la blogi mwezi Desemba 2017 ambalo lilitambua athari mbaya za kutumia mtandao miongoni mwa wateja wake

0 comments:

Post a Comment