Tuesday 21 August 2018

Hawa ndio wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa kiume UEFA



Mohamed Salah, Cristiano Ronaldo na Luka Modric wametajwa katika orodha ya wachezaji watatu wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa kiume wa UEFA kwa mwaka 2017/18
-
Salah ametajwa kwenye orodha hiyo baada ya timu yake ya Liverpool kumaliza katika nafasi ya pili kwenye michuano ya ligi ya UEFA msimu uliopita na kuifungia timu hiyo magoli 44 kwa msimu mzima
-
Ronaldo ametajwa kwenye orodha hiyo baada ya kushinda mataji matano ya UEFA na kumaliza mfungaji bora kwenye ligi hiyo kwa misimu 6 mfululizo
-
Aidha, Modric ambaye anatajwa kuwa na msimu mzuri katika klabu ya Real Madrid amefanikiwa kumaliza katika nafasi ya pili akiwa na timu yake ya Taifa kwenye Kombe la Dunia na yeye kushinda tuzo ya mchezaji bora

0 comments:

Post a Comment